Habari zetu wadau,
Natumaini kila mtu yuko poa, sasa
waswahili husema biashara asubuhi jioni mahesabu sasa ikiwa mwaka ndio
kwanza bado unanukia upya nimeona niwape habari hii. Natafuta wasichana
au wadada 3 ambao wanajua kurap au kuchana kwa vijana wanavyosema kwa
uzuri kabisa na kunata na beat. Wasicha hao wawe kwanza na mwonekano wa
kisanii na wawe na kipaji kweli chakuchana FREE STYLE. Shindano hilo
litaanza tarehe 14.1.14 hadi tarehe 24.1.14
Ili kushiriki shindano hilo kwanza unatakiwa uwe mtumiaji wa Instagram ambapo utatakiwa kufollow account ya @chokadj www.instagram.com/chokadj
halafu utajirecord video itakayokuwa inakuonyesha kufreestyle kitu
chochote kwa lugha ya Kiswahili na English kwa second 16 na kisha
utaweka hash tag hii #ChokaNaFreeStyle2014 halafu utaituma kwenye
account yako ya Instagram, mdada atakayepata LIKE nyingi kwenye hiyo
clip ndio atakuwa ananafasi kubwa yakushinda.
Shindano hili ni kwa wadada wanaoishi DAR
ES SALAAM Pekee, washindi hao watatu wataingia katika mixtape yangu na
watarekodi wimbo wao wa pamoja pale B’HITZ STUDIO na pia watafanyiwa
video ya wimbo huo na pia watapata PROMO ya kazi zao kupiti website hii
ya DJCHOKA MUSIC.
0 comments :
Post a Comment