
Klabu ya Manchester United ipo katika
mazungumzo na mshambuliaji,Wayne Rooney kwaajili ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka mitano.
Rooney amepewa ofa hiyo na mabingwa watetezi hao na iwapo atakubali kusaini mkataba huo atapewa unahodha pamoja na kuongezewa mshahara katika klabu hiyo.
Muingereza huyo kwa sasa anapokea kiasi cha pauni 250,000 kwa wiki hivyo mshahara wake utaongezwa na kufikia pauni 300,000 kwa wiki.
Uhamisho wa Juan Mata kutoka klabu ya Chelsea huenda ukamvutia Rooney kukubali ofa hiyo mara baada ya siku zilizopita kusema kuwa anampango wa kuondoka klabuni hapo endapo uongozi hautasajili wachezaji wenye majina makubwa na kushindwa kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya.
0 comments :
Post a Comment