ZAHA NA JONES KUMFUATA SOLSKJAER CARDIFF

Zaha na Jones kumfuata Solskjaer Cardiff.Winga wa timu ya vijana ya
Uingereza,Wilfried Zaha atajiunga na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kwa mkopo katika kipindi chote kilichobaki cha msimu huu kwa kiasi cha pauni milioni 1.5.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amecheza michezo minne pekee na klabu ya Manchester United mmoja ukiwa wa ngao ya jamii waliposhinda dhidi ya Wigan.
Kuelekea kusini kwa Wales kutamfanya mchezaji huyo wa zamani wa Crystal Palace kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Huku Theo Walcott akiwa majeruhi na kukosa matumaini ya kucheza Kombe la dunia,Zaha atakuwa na matumaini ya kumshawishi meneja wa England,Roy Hodgson kumuita wakati akijaribu kuimarisha kiwango chake akiwa kwa mkopo Cardiff.
Pia mshambuliaji wa Stoke City,Kenwyne Jones naye anaelekea Cardiff katika dili ambalo mchezaji wa Nigeria,Peter Odemwingie atabadilishana na Muingereza huyo.

Jones alionyesha kila dalili ya kutaka kuiacha klabu hiyo mapema mwezi huu alimtumia meneja wake,Mark Hughes ujumbe wa meseji usiku ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza waliofungwa goli 5-3 na Liverpool Januari 12 kuwa hatokuwepo katika mchezo huo.
Mshambuliaji huyo alisisitiza kuwa amevutiwa kwenda Cardiff na atajaribu kuisaidia ibaki katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Wachezaji hao wote wawili kwasasa wapo St George’s Park kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
 

CONVERSATION

0 comments :

Post a Comment

Back
to top